Baada ya kutoka Arusha mjini, Kiteto na Loliondo Jukwaa lilihamia Zanzibar na ratiba ya Jukwaa ilitoka na kujadiliwa katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, VUGA Zanzibar siku ya Jumamosi Tarehe 07 na 08 Februari 2009.
Mada zilizojadiliwa katika Jukwaa la Zanzibar lililofanyika Tarehe 07 na 08 Februari 2009.
Jumamosi (07 Februari 2009)
Mada zilizojadiliwa katika Jukwaa la Zanzibar lililofanyika Tarehe 07 na 08 Februari 2009.
Jumamosi (07 Februari 2009)
- Mfumo wa serikali za Mitaa, Zanzibar (Nafasi ya kijana katika vikao vya utoaji maamuzi)
- Nafasi ya kijana katika MKUZA.
Jumapili (08 Februari 2009)
- Sera ya Vijana, Zanzibar.
Jukwaa hilo lililofanyika likiwa na lengo la kujenga mahusiano na ushirikiano bora baina ya jumuiya za vijana Tanzania pamoja na serikali kwa lengo la kuondoa matatizo yanayomkabili kijana ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini liliweza kukutanisha vijana themanini na tisa(89) kutoka kwenye mashirika mbali mbali. Ripoti ya jukwaa imetoka na itakuwa katika blog yako muda si mrefu ili na wewe uweze kutoa maoni yako.