Monday, February 2, 2009

Jukwaa la Loliondo 25-26/11/2008

Warsha ya utawala bora na ushirikishaji wa uma katika kufanya maamuzi loliondo 25-26/2008

TYC ilifanya warsha ya utawala bora katika kijiji cha loliondo katika kitongoji cha wasso tarehe 25-26/11/2008,warsha hiyo ilihudhuriwa na vijana wapatao 100 kutoka pande mbalimbali za loliondo ikisimamiwa kwa ukaribu kabisa na ngorongoro Network (NGONET)ambayo ni asasi shiriki ya TYC loliondo

Mkutano ulichukua siku mbili ambapo siku ya kwanza mwezeshaji alipata wasaa wa kutembelea vikundi na kuweza kushawishi kikundi kimoja kujiunga na TYC. Siku ya pili kulikuwa na warsha ambayo ilikuwa inazungumzia mambo ya Utawala Bora.

Utawala Bora
Utawala bora huanza katika ngazi ya chini kabisa na kutanuka hadi ngazi ya juu au kubwa kama ifuatavyo.Binafsi,familia /kaya kitongoji/jamii, kata,tarafa,wilaya,mkoa,kanda,taifa,kimataifa

Vigezo vya Utawala Bora
Uwazi,demokrasia,uadilifu,ukweli usawa,ushirikishwaji,uaminifu,uzalendo mawasiliano,msimamo haki

Baada ya kujadili kwa kupitia njia mbalimbali za kuwezesha uwepo wa utawala bora washiriki walipendekeza kwamba TYC(Asasi iliyoanda warsha) na NGONET(Asasi shiriki) waongeze warsha katika nyanja mbalimbali ili kuwakomboa vijana ili kuwajengea ufahamu.