Tuesday, January 27, 2009

Jukwaa la vijana: An opportunity to influence!

Karibuni katika blog ya jukwaa la vijana ambayo itakuwa inawaletea habari na taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo ya vijana nchini. Blog ya jukwaa la vijana itakupa fursa ya kufahamu nini kimejiri katika vikao vya majukwaa ya vijana ambayo yanaendeshwa katika wilaya 4 za Arusha mjini, Kiteto, Ngorongoro na Kinondoni. Jukwaa la vijana Zanzibar tayari limeshazinduliwa mnamo tarehe 17/01/2009. Juhudi zinafanywa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanashiriki katika wilaya 5 zaidi mwaka 2009 zikiwemo Pwani, Mtwara mjini, Lindi mjini, Masasi na Ruangwa.

Karibuni kwa maoni na maboresho... Vijana tunaweza tukiwezeshwa na kujiwezesha!

KARIBUNI

Tanzania Youth Coalition (TYC) pamoja na wabia wake wa majukwaa inawaletea njia rahisi ya kupata taarifa kupitia mtandao. Hii itasaidia kwa wale wote wasioweza kuhudhuria vikao vya majukwaa kupata taarifa kirahisi na kuweza kutoa maoni juu ya yaliyojili katika majukwaa mbalimbali!

Kaa mkao wa kula!