Thursday, May 28, 2009

......Mwezi wa November ndio huu vijana tujiandaeee...........

Up to know the Tanzania Youth Coalition (TYC) has been able to start and organise about 9 distict platform all over Tanzania From Lindi, Ruangwa, Masasi, Mtwara urban, Kiteto, Loliondo, Arusha Urban to Zanzibar and soon we will also start youth platform in the district of Mbeya, Iringa and Morogoro, where by in these Platform about 100 youth from these are meets together with some officials from the Local Government Authority so as they could discuss, inform one another and share views with the local officials as a way of making sure that, what happens in their area is well known by the community that surrounds. These meetings are held Quartey in a year that to mean the meetings are held after every three months from January, March, June and September.

Hongera kwa majukwaa yaliyoanza na yanayoendelea kwani baada ya majukwaa kufanyika hapo mwezi wa nne na wa tano, majukwaa awamu ya tatu yanakuja mnamo mwezi wa sita ikiwa ni katika kufuata kalenda ya mpango mzunguko ya serikali za mitaa. Kalenda hiyo imeainisha kukaa kwa vikao vinne vya msingi kwa mwaka kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa, ngazi ya wilaya, ngazi ya Halmashauri (Mkoa) na ngazi ya mwisho ni ngazi ya utekelezaji wa yote yaliyokubaliwa katika ngazi zote hapo kabla.
Awamu hii vijana watakutana na kujadili jinsi gani ya kushawishi na kupenyeza mawazo yao katika ngazi ya halmashauri ikiwa ni kabla ya bunge la bajet kukaa hapo baadae! Wadau mnakaribishwa kwa maoni na kwa wale wenye mawazo ya nini wanashauri kipelekwe kwa vijana ikiwa ni katika kujengeana uwezo na kufanya nchi yetu iweze kupiga hatua wanakaribishwa kupitia barua pepe info@tyctz.org na tycoalition@yahoo.com,

.............................Vijana tukiwezeshwa tunaweza.....................................................

Yaliyokuwa yanajiri kipindi cha kuchagua vijana watakao wawakilisha wenzao katika jukwaa...


Pata kuona moto uliowashwa na TYC na vijana kupokea kwa ari ujumbe uliopelekwa kwao na TYC. Vijana wa Masasi wako juuuuu
The video potray the true filling of the youth from Masasi who wanted to represents others from the youth platforms in sending the Masasi youth views in the Ward District Council meetings.

Monday, May 25, 2009

Increasing communication with the youth from the Platforms..........

Karibuni kwa maoni na ushauri juu ya jinsi gani ya kuboresha majukwaa yetu haya ya vijana ili kuhakikisha taarifa sahihi zinasambaa kwa vijana na kuhakikisha lile lengo mahususi la majukwaa linafikiwa.

Hellow youth and all that are interested in knowing the news about these Youth Platforms that are taking place in over eight (8) districts Country wide, would also like to hear or receive your comments on what should be added to make sure these platform gets better and better!

You are all welcome KARIBUNIIIIIIII!
Blog Master.

Saturday, May 23, 2009

KERO MAHUSUSI ZILIZOKUWA ZIKITOLEWA NA VIJANA!

Vijana walioshiriki katika majukwaa ya vijana kuanzia Lindi, Ruangwa, Masasi, Mtwara Mjini, Zanzibar, Arusha Mjini, Kiteto na hata Loliondo wameonesha kuwa ni wamoja japokuwa wanatenganishwa na maeneo waishiyo au kufanyia kazi, kwani mambo ambayo yamekua yakiwasibu au kuwakumba katika kuwainua au kuwakandamiza kimaisha yamekuwa yakifanana katika maeneo yote yaliyofikiwa katika awamu hii ya majukwaa ya vijana. Japokuwa kutokana na uhalisia wa sehemu hizi pia kumekuwa na tofauti kidogo katika changamoto zingine. Vijana hawa wote wamekuwa wakikumba na kero za kimsingi zipatazo tano (5) ambazo ni:
  1. Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika serikai za mitaa.
  2. Kukosa Elimu ya Ujasiriamali.
  3. Upungufu wa maeneo ya kufanyia biashara na masoko
  4. Ugumu wa upatikanaji wa mikopo kutokana na vijana wengi kushindwa kukopesheka kwa kukosa vitu kama dhamana.
  5. Upungufu au ukosefu wa SACCOS zaidi zile za Vijana katika maeneo haya.


Safari ikaamia na Mtwara mjini!
Hapa Vijana wa Mtwara wakisikiliza kwa umakini
mada zilizokuwa zinawasilishwa na mwezeshaji!










Pia vijana walikuwa na shughuli nyingi wakati wa majukwaa kwani pia walikuwa wakipewa kazi za makundi na kutakiwa kujadili masuala mbalimbali yanayowasibu wao kama vijana kutoka Mtwara mjini!

Mijadala ikawa inaendelea


Hapa tunaona jinsi vijana walivyokuwa wakishiriki katika jukwaa la vijana masasi na pia kama unavyoweza kuona katika picha ya kwanza mmoja kati ya vijana akiwaelezea vijana washiriki jinsi gani kama wakimpendekeza kuwa mwakilishi wao katika kamati ya Jukwaa ataweza kuwasaidia vijana wengine kupeleka mawazo yao mbele!

Mapicha kadha wa kadha kutoka katika majukwaa kuonyesha vijana wakiwakilisha mawazo yao.........











Monday, May 18, 2009

....:: :: Jukwaa la Vijana Arusha Mjini :: ::.......

Vijana mbalimbali kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Arusha Mjini walipata nafasi ya kukusanyika wao pamoja na viongozi baadhi kutoka serikali ya mtaa kuzungumzia maswala yanayomkabiri kijana kutoka maeneo hayo na kuibuka na kero pamoja na mapendekezo yafuatayo;

KERO
1. Kutodhaminika na kutothaminika (ajira na mikopo).
2. Kutokushirikishwa kwa vijana katika uundwaji na utekelezaji wa sera zinazowahusu.
3. Kutokua na elimu ya afya ya uzazi.
4. Ukosefu wa mawasiliano kati ya viongozi na vijana.

Na kutoa mapendekezo yafuatayo kulingana na kero hizo;

  1. Kujishirikisha na si kusubiri kushirikishwa kwenye shughuli za kimaendeleo na kijamii.
  2. Utungwaji wa sera za vijana na vijana wenyewe, kwani wao ndio wanaojua wanahitaji nini kwa muda gani na mazingira yapi, na sio kushushiwa tu sera na wakuu wa Mamlaka na wao kushiriki kwenya utekelezaji wakiwa kama washika dau wakuu.
  3. Vijana kupewa elimu ya biashara ili waweze kufahamu namna ya kuendesha biashara zao kwa ufasaha na pindi waombapo mikopo waweze kuandika michanganuo mizuri kwa ajiri ya biashara zao na kufanikiwa kupata mikopo.


..........Jukwaa la Vijana Zanzibar................

Vijana kutoka Tanzania Zanzibar walipata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yanayowahusu vijana wa kutoka kisiwani humo na kutoa kero pamoja na mapendekezo kulingana na kero hizo husika kama ifuatavyo:
KERO:
  1. Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika vikao vya serikali za mitaa.
  2. Vijana kukosa elimu ya ujasiriamali.
  3. Kutokuaminiwa kwa vijana katika kupewa mikopo.
  4. Vijana kukosa mazingira mazuri ya kufanyia na kuanzisha shughuli za kibiashara.
Na kupendekeza kwamba:
  1. Elimu ya ujuzi na ufundi ianze toka shule ya msingi.
  2. Vijana kupewa kipaumbele katika vyombo vya maamuzi kuanzia ngazi ya chini.
  3. Vijana kupatiwa mwakilishi katika baraza la wawakilishi.
  4. Vijana kupatiwa fursa mbalimbali za kijamii.

Friday, May 8, 2009

Majukwaa ya Kiteto, Loliondo na Arusha Mjini yapigiliwa msumari

Wawezeshaji kutoka Muungano wa mashirika ya Vijana yasiyokuwa ya Vijana Tanzania (TYC) warudi na kupiga msumari majukwaa ya Vijana yaliyoko Katika Mikoa ya Arusha na Manyara yaani Wilaya za Arusha Mjini, Kiteto na Loliondo. Katika kuhakikisha Vijana wa maeneo hayo wanakuwa na uelewa wa kutosha juu Sera ya maendeleo ya Vijana na Mpango kazi wa ajira kwa maendeleo ya vijana Tanzania na Mpango Mzunguko (Planning cycle) wa serikali za mitaa! Katika kuwaanda na raundi ya pili ya majukwaa hapo mwezi wa sita (6) mwaka huu!

Habari kutoka majukwaa ya Lindi, Ruangwa, Masasi na Mtwara Mjini

Vijana kutoka katika wilaya nne tofauti za Lindi Mjini, Ruangwa, Masasi na Mtwara Mjini walipata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yao pamoja na kupata kufahamu sera mbalimbali za vijana za kitaifa ambazo zilikuwa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 na Mpango kazi wa ajira na maendeleo kwa vijana na pia kupata kufahamu Mpango mzunguko(Planning cylce) wa Serikali za mitaa.

Pamoja na vijana kujadili na kupitia sera pia walipata wasaa wa kutoa kero zinazowasibu au kuwakumba katika wilaya hizo tofauti nne ambapo kero nyingi za vijana zilijikita katika maeneo mahususi matano (5)
  1. Ushiriki na Ushirikishwaji wa vijana katika Serikali za mitaaa.
  2. Ukosefu wa Elimu ya Ujasiriamali.
  3. Kukosekana kwa SACCOS ya Vijana.
  4. Ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara na masoko.
  5. Maswala mazima ya Kodi.