Vijana walioshiriki katika majukwaa ya vijana kuanzia Lindi, Ruangwa, Masasi, Mtwara Mjini, Zanzibar, Arusha Mjini, Kiteto na hata Loliondo wameonesha kuwa ni wamoja japokuwa wanatenganishwa na maeneo waishiyo au kufanyia kazi, kwani mambo ambayo yamekua yakiwasibu au kuwakumba katika kuwainua au kuwakandamiza kimaisha yamekuwa yakifanana katika maeneo yote yaliyofikiwa katika awamu hii ya majukwaa ya vijana. Japokuwa kutokana na uhalisia wa sehemu hizi pia kumekuwa na tofauti kidogo katika changamoto zingine. Vijana hawa wote wamekuwa wakikumba na kero za kimsingi zipatazo tano (5) ambazo ni:
- Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika serikai za mitaa.
- Kukosa Elimu ya Ujasiriamali.
- Upungufu wa maeneo ya kufanyia biashara na masoko
- Ugumu wa upatikanaji wa mikopo kutokana na vijana wengi kushindwa kukopesheka kwa kukosa vitu kama dhamana.
- Upungufu au ukosefu wa SACCOS zaidi zile za Vijana katika maeneo haya.
No comments:
Post a Comment