Vijana mbalimbali kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Arusha Mjini walipata nafasi ya kukusanyika wao pamoja na viongozi baadhi kutoka serikali ya mtaa kuzungumzia maswala yanayomkabiri kijana kutoka maeneo hayo na kuibuka na kero pamoja na mapendekezo yafuatayo;
KERO
1. Kutodhaminika na kutothaminika (ajira na mikopo).
2. Kutokushirikishwa kwa vijana katika uundwaji na utekelezaji wa sera zinazowahusu.
3. Kutokua na elimu ya afya ya uzazi.
4. Ukosefu wa mawasiliano kati ya viongozi na vijana.
Na kutoa mapendekezo yafuatayo kulingana na kero hizo;
- Kujishirikisha na si kusubiri kushirikishwa kwenye shughuli za kimaendeleo na kijamii.
- Utungwaji wa sera za vijana na vijana wenyewe, kwani wao ndio wanaojua wanahitaji nini kwa muda gani na mazingira yapi, na sio kushushiwa tu sera na wakuu wa Mamlaka na wao kushiriki kwenya utekelezaji wakiwa kama washika dau wakuu.
- Vijana kupewa elimu ya biashara ili waweze kufahamu namna ya kuendesha biashara zao kwa ufasaha na pindi waombapo mikopo waweze kuandika michanganuo mizuri kwa ajiri ya biashara zao na kufanikiwa kupata mikopo.
No comments:
Post a Comment