Friday, May 8, 2009

Habari kutoka majukwaa ya Lindi, Ruangwa, Masasi na Mtwara Mjini

Vijana kutoka katika wilaya nne tofauti za Lindi Mjini, Ruangwa, Masasi na Mtwara Mjini walipata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yao pamoja na kupata kufahamu sera mbalimbali za vijana za kitaifa ambazo zilikuwa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 na Mpango kazi wa ajira na maendeleo kwa vijana na pia kupata kufahamu Mpango mzunguko(Planning cylce) wa Serikali za mitaa.

Pamoja na vijana kujadili na kupitia sera pia walipata wasaa wa kutoa kero zinazowasibu au kuwakumba katika wilaya hizo tofauti nne ambapo kero nyingi za vijana zilijikita katika maeneo mahususi matano (5)
  1. Ushiriki na Ushirikishwaji wa vijana katika Serikali za mitaaa.
  2. Ukosefu wa Elimu ya Ujasiriamali.
  3. Kukosekana kwa SACCOS ya Vijana.
  4. Ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara na masoko.
  5. Maswala mazima ya Kodi.

No comments: