Tuesday, January 27, 2009

Jukwaa la vijana: An opportunity to influence!

Karibuni katika blog ya jukwaa la vijana ambayo itakuwa inawaletea habari na taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo ya vijana nchini. Blog ya jukwaa la vijana itakupa fursa ya kufahamu nini kimejiri katika vikao vya majukwaa ya vijana ambayo yanaendeshwa katika wilaya 4 za Arusha mjini, Kiteto, Ngorongoro na Kinondoni. Jukwaa la vijana Zanzibar tayari limeshazinduliwa mnamo tarehe 17/01/2009. Juhudi zinafanywa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanashiriki katika wilaya 5 zaidi mwaka 2009 zikiwemo Pwani, Mtwara mjini, Lindi mjini, Masasi na Ruangwa.

Karibuni kwa maoni na maboresho... Vijana tunaweza tukiwezeshwa na kujiwezesha!

2 comments:

Tanzania Youth Coalition said...

Congrats TYC, i think time has come that vijana wa Tanzania tusimame ili kuchangia mustakabali wa nchi yetu... If we dont do it by ourselves nobody will do it for us..

Cheers

Mdau

Anonymous said...

tunashukuru kwa kazi yenu tunaomba habari zaidi